Kimchupa MediaTz

NYUMBANI KWANZA

HEADLINE


https://a.msn.com/54/en-us/ct-6.7963,39.2847?weadegreetype=F&ocid=msedgntp

Jumatano, 25 Oktoba 2017

VIDEO: Daktari aibua mazito ya Kanumba

Mbele ya Jaji Sam Rumanyika leo Oktoba 25, 2017 katika mahakama kuu Kanda ya Dar es salaam, imemaliza kusikiliza ushahidi wa kesi namba 125/2012 inayomuhusu Msanii Elizabeth Michael maarufu kama 'Lulu' ya kumuua mpenzi wake Steven Kanumba bila kukusudia, ambapo kesho Oktoba 26 Mahakama hiyo itasikiliza maoni ya Baraza la wazee wa mahakama sambamba na kupanga tarehe ya hukumu.

Kwamujibu wa maelezo ya shahidi namba 2  na wa mwisho kwa upande wa mshitakiwa, aliyefahamika kama Josephine Mshumbus yaliyosomwa kwaniaba yake na Staff Sajenti wa polisi Detective E103 Aitwaye Nyangea, aliyotoa 23/04/2012, ameeleza kuwa yeye alimfahamu Marehemu Steven Kanumba Kama Mgonjwa wake katika kituo chake cha tiba mbadala cha Precious Clinic kilichokuwepo karibu na Jengo la Mawasiliano Jijini Dar es salaam.

 "Steven Kanumba alikuwa ana matatizo ya sumu mwilini na alikuwa anakuja kwenye kituo changu cha Kliniki Ambapo alikuwa akifanya vipimo vya mwili mzima na aligundulika kuwa na tatizo la Mafuta (Cholestrol), tatizo la Moyo, Upungufu wa Hewa ya Oksijeni kwenye Ubongo ambayo yalimsababishia maumivu makali.

TAZAMA FULL VIDEO HAPO CHINI YA LULU LEO MAHAKAMANI

Hakuna maoni: