Kimchupa MediaTz

NYUMBANI KWANZA

HEADLINE


https://a.msn.com/54/en-us/ct-6.7963,39.2847?weadegreetype=F&ocid=msedgntp

Ijumaa, 10 Februari 2017

WABUNGE NA MAWAZILI WAMUUNDIA TUME MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM POUL MAKONDA




SIKU chache baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, kutaja watuhumiwa 65 katika vita dhidi ya dawa za kulevya, Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kimesema haki zimekiukwa katika utajaji majina.

Mbali na LHRC baadhi ya wanaharakati wameungana na kituo hicho kukosoa utaratibu uliotumiwa na Makonda.

Akizungumza na gazeti hili jana, Mkurugenzi wa LHRC, Dk Hellen Kijo-Bisimba alisema kutangaza majina ya watu kwa kuwahusisha na dawa za kulevya bila uchunguzi, ni kinyume na  haki za binadamu na kuchafua majina yao kwa vile hakuna  uthibitisho wa kuwahusisha na tuhuma hizo.

Alisema hayo baada ya mwandishi wa habari hizi kumtaka azungumzie mazingira ya kutaja majina ya watuhumiwa kwa kulinganisha na misingi ya haki za binadamu.

Dk Bisimba alisema majina ya watu yalipaswa kutajwa kama Jeshi la Polisi nchini lingefanya uchunguzi wa awali na kupata uthibitisho na  Mahakama ndiyo yenye jukumu la kutoa haki kwa kutafsiri sheria na si kiongozi.

“Kama uchunguzi wa awali ungefanyika, suala la kutaja majina lingekuwa  sahihi, lakini  kutangaza bila upelelezi ni kinyume na sheria,” alisema.

Alisema Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro aliwahi kunukuliwa na vyombo vya habari akisema walipata kupokea majina ya uongo, hivyo ni hatari kutangaza jina la uongo kisheria.

Wakili wa Kujitegemea, Nassor Kitugulu alisema ni jambo la kushangaza mtu kutaja mbinu za adui, hiyo ni dalili kuwa vita hiyo ni ngumu bila ushirikiano.

Alisema iwapo Serikali imedhamiria kupambana na dawa za kulevya nchini baada ya kutambua njia zinazotumiwa, ilipaswa kuweka mitego ya kunasa watuhumiwa.

“Tunajua kuwa dawa za kulevya zinapoteza nguvukazi, lakini utaratibu wa kutangaza bila uthibitisho wa tuhuma ni kuchafua sifa ya mtu kwenye jamii,” alisema.

Naye Fidelis Butahe anaripoti kutoka Dodoma, kwamba Bunge juzi usiku liliweka historia kwa kupitisha maazimo manne, yakiwamo ya kumtaka Makonda na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Alexander Mnyeti kuhojiwa na Kamati ya Bunge ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge na ikibainika wana makosa mamlaka zao za uteuzi ziwawajibishe.

Wateule hao wa Rais wanadaiwa kutoa kauli za kudharau Bunge takribani siku tatu zilizopita na kuamsha hisia za wabunge waliotoa kauli za kuwakemea bungeni.

Kwa sakata hilo, Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara (Chadema) aliwasilisha hoja ya kutaka washughulikiwe, ambayo ilijadiliwa kuanzia saa 1.30 usiku hadi saa 2.15 usiku na kuungwa mkono na wabunge wote, wakiwamo mawaziri kwa kusema “ndiyo”.

Wakati wa mjadala wa hoja hiyo, Mbunge wa Bunda, Esther Bulaya (Chadema) alieleza jinsi Makonda alivyompigia simu kumweleza kuwa atawashughulikia wabunge, kwa sababu yuko karibu na ‘Bwana mkubwa’, huku Joseph Msukuma (Geita Mjini-CCM) akitangaza vita na Mkuu huyo wa mkoa.

Ilikuwa kama sinema bungeni, kutokana na wawakilishi hao wa wananchi kuonekana kama wabunge wa chama kimoja, walipotoa hoja zao kupinga kauli hizo, huku Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge akiwaongoza kufuata kanuni za chombo hicho katika mjadala huo.

Maazimio hao ni; Makonda na Mnyeti kuitwa mbele ya Kamati, Waziri wa Tamisemi kutoa maelekezo kwa wakuu wa mikoa na wilaya namna ya kufanya kazi zao bila kuingilia mihimili mingine.

Pia, mamlaka nyingine zikimhitaji Mbunge kwa mashitaka ya aina yoyote lazima zimjulishe Spika wa Bunge na mamlaka ya kinidhamu kuwawajibisha wateule hao wa Rais ikibainika wametenda kosa la kudharau chombo hicho.

Ilivyokuwa

Akiwasilisha hoja hiyo usiku baada ya kipindi cha asubuhi kutoruhusiwa na Chenge kwa maelezo kuwa alitaka kujiridhisha kama Mbunge huyo alizingatia kanuni, Waitara alisema Mnyeti ameonekana katika mitandao ya kijamii akisema wabunge hawajielewi.

“Haya mambo ndiyo yamejirudia wakati nikiangalia televisheni ya Clouds, Makonda akionekana akisema sisi humu bungeni tunasinzia,” alisema Waitara.

Alibainisha kuwa kwa mujibu wa Katiba ibara ya 63(2), Bunge ndicho chombo kikuu kwa niaba ya wananchi, kuisimamia na kuishauri Serikali na linapitisha bajeti inayotum.

Hakuna maoni: