Kimchupa MediaTz

NYUMBANI KWANZA

HEADLINE


https://a.msn.com/54/en-us/ct-6.7963,39.2847?weadegreetype=F&ocid=msedgntp

Jumatano, 15 Februari 2017

KAULI YA KIGWANGALLA JUU YA MASHOGA BAADA YA MADAWA YA KULEVYA MASHOGA WAJIANDAE DAR ES SALAAM NA NCHI NZIMA


         Naibu Waziri Wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangalla amesema kuwa atawaweka hadharani wanaume wote wanaojihusisha na mapenzi ya jinsi moja (mashoga) ambao hufanya biashara hiyo kupitia mitandao ya kijamii.

Naibu Waziri aliyasema hao jana usiku kupitia ukurasa wake wa Twitter ambapo alieleza kuwa yupo katika ziara jimboni kwake na mara atakaporejea jijini Dar es Salaam kabla ya kuhamia Dodoma rasmi ataiweka orodha hiyo hadharani.

Aidha, amesema kuwa wale wote wanaodhani kuwa vita dhidi ya wanaume wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja ni mzaha, wataona hali itakavyokuwa kwani vita hiyo ni kubwa sana na wataishinda.

Kigwangalla ambaye pia ni mtaalamu wa afya alisema kuwa suala la mtu kuwa shoga si suala la kibaolojia (asili) bali ni watu tu kujiendekeza na hivyo watakahikikisha wanalikomesha.

Sheria ya ndoa ya Tanzania inapinga watu wa jinsia moja kujihusisha na mahusiano ya kimapenzi, lakini pia ni kitu kilichozuiliwa katika vitabu vitakatifu vya dini

Hakuna maoni: